Friday, May 25, 2012


MNYIKA ASHINDA KESI YA UBUNGE MAHAKAMA KUU LEO


Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya Chadema, John Mnyika akiwa na aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu 2010,Hawa Nghumbi, wakati wakisubiri hukumu, katika Mashakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuhusu kesi  ya kupiga matokeo yaliyompa ushindi Mnyika iliyofunguliwa na Nghumbi kwenye mahakama hiyo.

BAADA YA KIPIGO CHA  SIMBA 5/O LLYOD NCHUNGA AACHIA NGAZI YANGA

Thursday, May 24, 2012
Baada ya vuta ni kuvute iliyogubika Klabu ya Yanga baada ya kukumbwa na mnikasa mingi ikiwemo kukumbwa na madeni na kufanya vibaya katika michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara iliyomalizika, aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Llyod Nchunga ameachia ngazi.
     Habari zilizoufikia mtandao huu zimesema Nchunga ametangaza uamuzi huo leo baada ya kinachoonekana maji kumfika shingoni.
    Hatua hiyo, Nchunga ameichukua baada ya wiki iliyopita, Wanachama wa Yanga wakiongozwa na Kamati ya Mwafaka ya Wazee wa timu hiyo kukutana klabuni hapo na kutangaza kumfukuza.
Hata hivyo baada ya hatua ya wanachama hao ilipingwa na baadhi ya wadau wa michezi ikiwemo TFF kwamba hawakufuata taratibu.

TBL YAMZAWADIA BAJAJI WAKALA BORA KANDA YA KASKAZINI


 Meneja  Usambazaji wa Wateja Wakubwa wanaouza bidhaa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kaskazini, Fortunatus Alfred  akimkabidhi kadi na funguo za bajaji yenye thamani ya sh. milioni 4,
Mary Kimario  ambaye ameshinda uwakala bora wa usambazaji na uuzaji wa bidhaa za TBL Kanda ya Kaskazini. Hafla hiyo ilifanyika  hivi karibuni mjini Moshi, Kilimanjaro.

 Meneja  Usambazaji wa Wateja Wakubwa wanaouza bidhaa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kaskazini, Fortunatus Alfred  akimkabidhi kadi na funguo za bajaji yenye thamani ya sh. milioni 4,
Mary Kimario  ambaye ameshinda uwakala bora wa usambazaji na uuzaji wa bidhaa za TBL Kanda ya Kaskazini. Hafla hiyo ilifanyika  hivi karibuni mjini Moshi, Kilimanjaro.
Mfanyakazi wa Mfanyabiashara ambaye amejishindia Uwakala bora wa bidhaa za Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Kaskazini, Mary Kimario akiwa kwenye bajaji yenye thamani ya sh. mil. 4 aliyozawadiwa. Wanaoshuhudia ni baadhi ya ndugu zake na wafanyakazi wa TBL.Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni mjini Moshi, Kilimanjaro.

BREAKING NEWS..MBUNGE WA ROMBO JOSEPH SELASINI APATA AJALI AMPOTEZA MAMA YAKE MZAZI

.

Mbunge wa Rombo Joseph Selasini (pichani) amepata ajali eneo la Bomang'ombe kata ya Hai ,Mjini baaday ya gari alilokuwa akiendesha yeye mwenyewe Toyota Land Cruzer lenye namba T 441 DRT kupinduka wakati akiwa anamkwepa mwendesha baiskeli.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa ajli hiyo imetokea majira ya saa 8;49 kuelekea saa 7 ambapo ndani ya gari hilo kulikuwepo na watu sita.

Chanzo cha ajali hiyo klimeelezwa kuwa ni mwendo kasi na pia mbunge huyo alipojaribu kumkwepa mwendesha baskeli ndipo gari hiyo ilipopinduka na kuua watu watatu akiwemo mmaa yake grlory shao na wengine watatu wakijeruhiwa vibaya.

Miiili ya watu waliopoteza maisha imepelekwa hospitali ya mkoa ya Mawenzi huku waliojeuhiwa wakipatiwa matibabu  hospitali ya wilaya ya hai.
You might also like:

Monday, May 21, 2012

Ushindi mtam

Featured Posts



KWELI DROGBA NI KIJOGOOOO!!!!!!!!!!

HAKUNA KAMA CHELSEA ULAYA, BAYERN WALIA ALLIANZ ARENA
Allianz Arena
Dider Drogba akishangilia.

Didier Drogba akiwa amenyanyua juu Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kocha wa Chelsea Roberto Di Matteo akishangilia ubingwa wa Ulaya

Wachezaji wa Chelsea wakishangilia na Kombe lao.
Bastian Schweinsteiger akiwa amejifunika uso baada ya kukosa Penati ya mwisho.

Mshambuliaji Didier Drogba kushoto, akishangilia kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya sambamba na kiungo Raul Meireles na Jose Bosingwa.

LONDON, EnglandMSHAMBULIAJI mkongwe na nahodha wa Ivory Coats, Didier Drogba, usiku wa kuamkia leo ameipa klabu yake ya Chelsea ya England ubingwa wa Ligi ya mabingwa Ulaya 2011 - 2012 alipoifungia bao la kusawazisha na baadaye kufunga penati ya mwisho iliyosababisha wawalaze Bayern Munich ya Ujerumani kwa penati 4-3, amesema ushindi huo umeipooza machungu yao ya 2008.
Akizungumza baada ya kutua jijini London, huku wakiwa na taji la kwanza la Ligi ya mabingwa Ulaya, Drogba alisema kuwa mwaka 2008 walinyongwa sana mjini Moscow wiliposhindwa na Manchester United katika fainali kwa mikwaju ya peneti.

Alisema baada ya kucheleweshwa sana hatimaye Mwenyezi Mungu ameamua kuwapa kile alichowapangia kwa muda mrefu na ambacho walicheleweshewa kukipata na kwamba sasa roho zao zimepoa.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuwezesha kuwa mabingwa Ulaya baada ya kucheleweshewa kwa muda mrefu, kwa kweli hii ni furaha tuliyoisubiri kwa muda mrefu,” alisema Drogba aliyetokwa na machozi baada ya kufunga penalti iliyowapa ubingwa.

Katika mchezo huo wa juzi timu hizo zilimalizi dakika 90 kwa sare ya bao 1-1, Munich ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia bao likifungwa na Thomas Müller katika dakika ya 83 lakini Didier Drogba akasawazisha katika dakika ya 88 na kusababisha timu hizo kuongezewa dakika 30 za nyongeza.

Katika dakika ya tano ya muda wa nyongeza Drogba alimkwatua Frank Ribery ndani ya eneo la hatari na mwamuzi akaizawadia penati lakini hata hivyo Arjen Robben, akashuhudia penati yake hiyo ikidakwa na kipa Petr Cech, katika dakika ya 95.

Baada ya kukosa penalti hiyo vijana wa Munich wakapoteza umakini na kujiamini na kuwapa Chelsea mwanya wa kufanya mashabulizi na kuutawala mchezo hadi dakika 15 za kwanza za muda wa nyongeza zilipomalizika na hata dakika 15 za mwisho mambo yaliendelea kuwa sare ya 1-1.

Baada ya kupigwa kura na kukukubaliana kulitumia goli la upande wa Kusini mwa uwanja, Bayern Munich ndio walioanza kupiga mikwaju ya penalti ambapo nahodha wake Philipp Lahm alifunga kabla ya Juan Mata wa Chelsea kupoteza, Mario Gomez akaifungia Munich penalti ya pili na David Luiz akaifungia Chelsea penalti ya kwanza kisha Manuel Neuer akaipa Munich penalti ya tatu na Frank Lampard akaifungia Chelsea penalti ya pili, Ivica Olic akaikosesha Munich penalti na Ashley Cole akafunga kufanya matokeo yawe penalti 3-3, Bastian Schweinsteiger akakosa penati ya tano ya Munich na Didier Drogba akafunga penati ya mwisho ya Chelsea hivyo matokeo kuwa 4-3.

Hilo limekuwa taji la kwanza Chelsea na imethibitisha kuwa ingali juu ya Bayern Munich kwani mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana ilikuwa mwaka 2005 katika robo fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya ambapo Chelsea ilishinda kwa jumla ya mabao 6-5 ya ugenini na nyumbani.

Wachezaji wa Chelsea waliokuwa kwenye kikosi hicho wakati huo na ambao hivi karibuni waliipa taji la Kombe la FA ni pamoja na Petr Cech, John Terry, Ashley Cole, Frank Lampard na Didier Drogba ambao pia wote walishiriki katika mechi hiyo.

Kwa kipigo hicho Bayern Munich ilishindwa kuungana na Liverpool kutwaa taji hilo kwa mara ya tano ikiwa imezidiwa na Real Madrid ya Hispania na AC Milan ya Italia, Munich walishindwa kuendeleza umwamba wa klabu za Ujerumani kuzitambia zile za England zilipopambana kwenye fainali ya Ligi ya mabingwa Ulaya.

Aidha hilo limekuwa pigo kwa kocha wa Munich, Jupp Heynckes, ambaye alishindwa kuingia kwenye rekodi ya kuwa kocha wa 19 kushinda kombe hili mara mbili, kwani alilitwaa mwaka 1998 alipokua akiinoa Real Madrid.





ILIKUWA NI SIKU YA MAJONZI!!

Mwenyekiti wa PR Promotion akiwa na msanii wa Maarufu Rehema Tajiri wakimlilia mafisango viwanja wa TCC Mafisango bado tunamkumbuka
MAJUKUMU MAZITO"

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kipya,Sunday Mangu ‘Linex’ amempa mchezaji filamu Wema Sepetu, jukumu la kusimamia video ya wimbo wa Aifola Ifola. Alisema kuwa ameamua kumkabidhi mwanadada huyo program zake zote kwa lengo la kuhakikisha video hiyo inakuwa nzuri

Thursday, May 17, 2012

WIZARA YA MALIASILI NA UTALII TAARIFA KWA UMMA:HAMNA KASHFA MPYA MALIASILI



1)Wizara ya Maliasili na Utalii imekanusha habari iliyoandikwa na gazeti moja la kila wiki lililotoka tarehe 15 Mei 2012 kwa kichwa cha habari ‘Kashfa mpya Maliasili’ zinazohusu ugawaji wa vitalu kwenye maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori (Wildlife Management Areas -WMAs).Wizara haihusiki na ugawaji wa vitalu ambao uliripotiwa na gazeti hilo kwa kuwa maeneo ya WMA yako nje ya Mapori ya Akiba ambayo ndiyo yanasimamiwa na Wizara moja kwa moja.
Gazeti hilo linanukuu tangazo ambalo lilitolewa na Muungano wa Jumuiya Zilizoidhinishwa za Hifadhi za Maeneo ya Wanyamapori Tanzania (Authorized Associations AAs Consortium) kuhusu vitalu. Tangazo hilo ambalo lilitolewa kwa njia ya magazeti liliwataka wadau wapeleke maombi ya vitalu vya uwindaji wa kitalii vilivyoko katika Maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) kwa kipindi cha mwaka 2013 hadi 2018 .

Inasisitizwa kuwa tangazo hilo la vitalu halikutolewa na Wizara wala Wizara haikuhusishwa kwa vyovyote vile katika kuandaa tangazo hilo. Hivyo, habari iliyotolewa na gazeti hilo  la kila wiki baada ya tangazo hilo kuchapishwa kuwa ugawaji wa vitalu vya WMA ni ‘Kashfa mpya Maliasili’ siyo kweli.
Tangazo lililotolewa na Muungano wa Jumuiya Zilizoidhinishwa za Hifadhi za Maeneo ya Wanyamapori Tanzania (Authorized Associations- AAs Consortium) siyo sahihi kwani Kifungu cha 31 (7) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5

2)ya mwaka 2009 kilichonukuliwa katika Tangazo hilo hakikuzingatiwa ipasavyo kwa misingi ifuatayo:-
       i.            Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori hakushirikishwa na hakutoa ridhaa yake  kabla ya tangazo hilo kutolewa;

     ii.            Halmashauri za Wilaya viliko vitalu hivyo nazo hazikushirikishwa; na

  iii.            Kifungu hicho [31(7)] hakitoi mamlaka kwa Muungano wa Jumuiya Zilizoidhishwa (Authorized Associations-AAs Consortium) kutoa tangazo la vitalu vya uwindaji wa kitalii katika Maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori (WMAs).

  iv.            Kanuni zinazotumika sasa hazitoi utaratibu utakaotumika kupata wawekezaji katika vitalu vya uwindaji wa kitalii vilivyoko katika WMAs. Kanuni za WMAs zinafanyiwa marakebisho na zitakapokamilika zitatoa utaratibu utakaotumika katika kutangaza vitalu vilivyopo kwenye WMAs.
Kutokana na sababu hizo Wizara ya Maliasili na Utalii inatahadharisha kuwa tangazo hilo siyo sahihi kwa kuwa halikuzingatia sheria. Kwa hiyo wadau wa uwindaji wa kitalii wanatahadharishwa kutopeleka maombi ya vitalu hivyo.
Wizara imewasiliana na Muungano wa Jumuiya Zilizoidhinishwa za Hifadhi ya Maeneo ya Wanyamapori Tanzania (Authorized Associations - AAs Consortium) kuwataka wasitishe mchakato huo wa kugawa vitalu katika maeneo ya WMA.
Wizara inazitaka Jumuiya za Hifadhi ya Wanyamapori (WMAs) kuwasiliana kila zinapotaka kutekeleza masuala yoyote yanayotawaliwa na sheria maana Wizara ndiyo yenye dhamana ya kusimamia Sera na Sheria za Wanyamapori.

George Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
16 Mei 2012

WACHEZAJI WAMLILIA MCHEZAJI MWENZAO MAREHEMU PATRICK MAFISANGO ALIYEKUFA KWA AJALI USIKU WA KUAMKIA LEO

 Mkurugenzi wa mtandao wa Fullshangweblog Bw. John Bukuku kulia akimsikiliza Katibu Mkuu wa timu ya Simba Bw. Evodius Mtawala wakati alipokuwa akielezea mipango ya kuuhifadhi na kuusafirisha mwili wa mchezaji wao marehemu Patrck Mafisango Mutesa aliyeafiki alfajiri ya usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chang'ombe Veta jijini Dar es salaam,  wakati akirejea nyumbani kwake na kusababisha watu wengine aliokuwa nao kupata majeraha.

Bw. Mtawala amesema hayo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili na kueleza kwamba kwa sasa wanawasiliana na Ubalozi wa Rwanda na mashirika ya ndege ili kukamilisha utaratibu wa vibali mbalimbali tayari kwa kuusafirisha mwili wa marehemu kwenda nchini Rwanda kwa mazishi na taarifa kamili ya lini utasafirishwa itatolewa kesho mara baada ya kukamilika kwa taratibu zote, katika picha kushoto ni Bw. Mwakitalima  mmoja wa mashabiki wa Simba aliyefika muhimbili kushuhudia kilichotokea.
 Mchezaji wa timu ya Simba Haruna Moshi Boban akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na jamaa na marafiki baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzao marehemu  Patrick Mafisango katika hospitali ya taifa ya Muhimbili .
 Wachezaji Haruna Niyonzima wa Yanga kushoto na Uhuru Selemani wa Simba wakisikitika wasijue la kufanya baada ya kushuhudia mwili wa mchezaji mwenzao marehemu Patrick Mafisango  katika chumba cha kuhifadhia maiti muhimbili leo.
 Mbunge wa jimbo la Korogwe CCM Steven Ngonyani Prof Maji  Marefu akizungumza na wanahabari hospitalini hapo kuelezea masikitiko yake juu ya kifo cha mchezaji huyo.
 Haruna Moshi akitoka kwenye chumba cha kuhifadhia maiti huku akilia kwa uchungu baada ya kuhakikisha kweli mwenzao Patrick Mafisango amefariki.
 Hapa Haruna Moshi akihojiwa alijaribu kuongea lakini akashindwa.
 Mchezaji Uhuru Selemani akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na mmoja wa waombolezaji.
 H
 Mchezaji wa zamani wa Simba Boniface Pawasa akilia kwa uchungu huku akifarijiwa na Mchezaji haruna Niyonzima wa Yanga, Pawasa amesema jana walikuwa naye kwenye muziki katika klabu ya Maisha Oysterbay wakati bendi ya Akudo Impact ikifanya onyesho klabuni hapo na marehemu alimuaga kwamba anaenda nyumbani baadae akapigiwa simu kwa simu ya marehemu akiambiwa mwenye simu hii amefariki dunia kwa ajali.
 Boniface Pawasa kushoto, Uhuru Selemani wakilia.
 Uhuru Selemani akisalimiana na wanamuziki wa bendi ya Akudo Impact ambao pia wameelezaea masikitiko yao kwani wamesema marehemu walikuwa naye usiku wa kuamkia leo katika klabu ya Maisha ambako walikuwa wakifanya onyesho lao.
 Aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Simba Mrundi Ramadhana Wasso akihojiwa na waandishi wa habari kuelezea masikitiko yake kutokana na msiba huo.
 Mashabiki wa Simba wakiwa katika hospitali ya Muhimbili kwa masikitiko makubwa kwa kuondokewa na mchezaji wao kipenzi.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili leo asubuhi.kwa hisani ya blog ya Fullshangwe

Shibuda: Hakuna urais bila kuchaguliwa na CCM


MBUNGE wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda ameeleza kuwa aliamua kutangaza nia ya kugombea urais Chadema kupitia vikao vya CCM kwa sababu anatambua kuwa hakuna mwanachama wa chama chake anayeweza kuwa Rais bila kuchaguliwa na chama hicho tawala.

Hata hivyo, jana Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limemshukia na kumtaka aeleze anafanya nini katika chama hicho kama anaamini kuwa hakiwezi kushika dola.

Shibuda alikaririwa na vyombo vya habari jana akieleza kuwa anataka kugombea urais kupitia Chadema na kumwomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuwa meneja wake.

Jana, alipotakiwa kufafanua zaidi mantiki ya kauli yake hiyo aliyoitoa wakati akiwasilisha mada kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) mjini Dodoma, Shibuda alisema anataka kuwa Rais wa Watanzania wote hivyo, hata kura za CCM anazihitaji ndiyo maana akatangaza mbele ya jukwaa lao.
Shibuda alisema hakuna mwanachama wa Chadema anayeweza kuwa Rais wa nchi hii bila kupata kura za baadhi ya wanachama wa CCM na Watanzania wengine: “Hata katika hayo majimbo ambayo Chadema tumeshinda, hatukupigiwa kura na wanachama wa Chadema pekee, bali walikuwepo hadi wa CCM wanaopenda mageuzi.

"Mimi ni ‘field marshal’ katika siasa. Ndiyo, nimetangaza mbele ya jukwaa la CCM kwa sababu nahitaji kura zao. Nahitaji kura ya Kikwete na wana CCM wengine, mimi siyo mtu mwoga wa kutangazia vichochoroni Kariakoo," alitamba Shibuda na kuongeza:

“Mtu pekee mwenye boresho la kisiasa ni Shibuda. Mimi ndiye ninayeweza kujenga umoja na kutimiza malengo ya nchi. Ndiyo maana nilimwambia Rais Kikwete sasa ni zamu yangu na nitakangaza mbele ya jukwaa la CCM siyo kujificha vichochoroni Kariakoo.”

Shibuda akitetea msimamo wake, alisema si dhambi kwa mhadhiri wa Kiislamu kwenda kutoa mahubiri ya kutoa uchafu wa roho mbele ya jukwaa la Wakristo vivyo hivyo, kwa mhadhiri wa Kikristo kwenda kutoa mahubiri kwenye jukwaa la Waislamu na kuhoji: “Kuna uharamu gani au je, ni usaliti kwa dini yake?”

“Tuache fikra finyu. Shibuda anataka kuwa Rais wa Watanzania wote. Wanaosema kwa nini nimeongea kwenye jukwaa la CCM wana fikra finyu. Mimi nina maono mapana ya kitaifa. Kwani hata watu waliotalakiana bado wanashirikiana kwenye misiba na harusi, wanakutana na kusalimiana na hawana ugomvi wowote, hao ndiyo watu wastaarabu. Tuache kuzusha mambo kwa hisia hasi.”

“Mfumo wa vyama vingi siyo uadui. Mimi nitakuwa Rais bora mwenye maono mapana ya kitaifa. Mimi ni sawa na gogo la udi likichomwa linatoa manukato. Nitaendelea kutangaza msimamo wangu na kuomba kura hata nikiwa katika jukwaa la NCCR-Mageuzi, CUF na vyama vingine kwani mimi nataka kuwa Rais wa Watanzania wote siyo wa kabila fulani au watu fulani. Mimi sibagui dini, kabila wala rangi. Watu waache fikra na mawazo mgando.”

Kauli ya Bavicha
Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche imesema baraza hilo limepokea kwa mshtuko taarifa kwamba Shibuda atagombea urais na meneja wake wa kampeni atakuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na alitoa kauli hiyo kwenye kikao cha Nec ya CCM.

Pia wameshtushwa na kitendo cha Shibuda kusema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuiongoza nchi kwa sasa na kutoa tamko hilo kwa niaba ya Taasisi inayotathmini Utawala Bora Afrika (APRM).

“Mambo hayo manne ndiyo yametushtua na kutufedhehesha sisi vijana wa Chadema na ndiyo maana, tumelazimika kutoa kauli kuhusiana na suala hili,” alisema Heche.

Heche alisema kamwe Bavicha haitaruhusu mgombea urais wa Chadema kuwa na meneja wa kampeni kutoka CCM akisema kina watu wa kutosha na wenye uwezo wa kufanya kazi hiyo.

“Kamwe hatutaruhusu mgombea urais wa Chadema awe anatangaza nia kwenye vikao vya CCM, kwani hawana mamlaka ya kumteua mgombea wa Chadema na kama Shibuda alikuwa halijui hilo anapaswa kulifahamu kuanzia sasa kuwa vijana wa Chadema hatuchaguliwi mgombea na Nec ya CCM kwani Chadema kuna vikao na taratibu zetu za kuteua wagombea,” alisema Heche.

Alisema kitendo cha Shibuda kusema kuwa hakuna chama kingine chenye uwezo wa kuongoza nchi ni kudhalilisha vijana wa Chadema na Watanzania wote ambao leo wanakiona chama hicho kama tumaini pekee la kuwakomboa.

“Kwa kauli hii, tunaamini kuwa mamlaka za nidhamu hazitakaa kimya bila kutakiwa maelezo ya kina. Tutaitisha kikao cha Baraza na tutaijadili kauli hii na kuwasilisha mapendekezo yetu kwenye vikao halali vya chama,” alisema na kuongeza:

“Kwa nini atafute urais kwenye chama ambacho anaona hakiwezi kuongoza dola? Anawatania Watanzania? Ni heri akaenda kwenye hicho ambacho anaamini kuwa kinaweza kuongoza dola. Kwani lengo la chama chochote kile ni kuchukua dola na si vinginevyo.”

ILIKUWA NI HEKAHEKA PALE Balozi wa Marekani alipokwama kwenye lifti

Balozi wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt (nyuma) akiwa amekwama kwenye lifti ya jengo la Wizara ya Nishati na Madini, jijini Dar es Salaam jana, alipokwenda kumtembelea Waziri wa wizara hiyo, Prof Sospeter Muhongo. Picha ndogo watu waliokuwemo kwenye lifti hiyo wakijalibu kufungua kwa mkono baada ya kukwama. Picha na Michael Jamson

NI KATIKA JENGO LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI, WAZIRI AMWOMBA RADHI
Na James Magai wa Mwananchi
BALOZI wa Marekani nchini, Alfonso Lenhardt jana alikwama ndani ya lifti katika Jengo la Wizara ya Nishati na Madini, Dar es Salaam kwa takriban dakika 20.

Balozi Lenhardt akiwa na ujumbe wake wa watu wawili, walikumbwa na mkasa huo mchana wakati wakienda kukutana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. Mbali na Balozi Lenhardt na ujumbe wake, pia kulikuwamo na watu wengine wakiwemo maofisa wa wizara hiyo na kufanya jumla ya watu saba kukwama kwenye lifti hiyo.

Saa 7:58 mchana mwandishi wetu alipofika wizarani hapo, alimkuta balozi huyo na wenzake hao wakiwa wamekwama ndani ya lifti hiyo katika ghorofa ya kwanza huku ofisa wa mapokezi wizarani hapo akihangaika kufanya mawasiliano na mafundi.

Mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo alifanikiwa kuifungua na kuacha uwazi wa kama sentimita 10 na kisha kuweka kibao ambacho kiliifanya iwe wazi lakini bila ya kuwawezesha waliokuwamo ndani kutoka.
Hatua hiyo iliwawezesha Balozi huyo na wenzake walau kupata hewa wakati wakisubiri hatua zaidi za kuwakwamua. walibaki humo hadi ilipotimu saa 8:14 mchana walipokwamuliwa baada ya mafundi waliokuwa wamefika muda mfupi kabla, kufanikiwa kuifungua.

Kutokana na tukio hilo, mkutano wa Balozi huyo na Waziri Profesa Muhongo uliokuwa umepangwa kuanza saa 8:00 ulichelewa kwa zaidi ya nusu saa kusubiri wageni hao wakwamuliwe. Ingawa hakuna ofisa wa wizara hiyo aliyekuwa tayari kuzungumzia mkasa huo wa kukwama kwa lifti hiyo, ilielezwa kwamba tatizo hilo limetokana na lifti hiyo kuwa mbovu.

Mmoja wa wafanyakazi wa wizara hiyo ambaye hata hivyo, jina lake halikuweza kupatikana mara moja alisikika akisema kuwa lifti hiyo ina kawaida ya kukwama.

Baada ya kufanikiwa kutoka, Balozi huyo na maofisa aliokuwa ameambatana nao pamoja na maofisa wengine wa wizara waliingia katika chumba cha mkutano na kuendelea na mazungumzo.
Hata hivyo, kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo, Waziri Profesa Muhongo alimtaka radhi Balozi Lenhardt na ujumbe wake kwa tukio hilo lakini akamtania kuwa bila shaka amepata uzoefu wa tatizo la nishati nchini, maelezo ambayo Balozi huyo aliyeitikia huku akicheka.

Ziara ya Balozi Lenhardt na ujumbe wake wizarani hapo ilikuwa na lengo la kumpongeza Profesa Muhongo kwa kuteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo na kuangalia jinsi ambavyo Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania kuboresha sekta hiyo.

Katika mazungumzo hayo ambayo pia yalihudhuriwa na Manaibu Waziri wa wizara hiyo, George Simbachawene na Stephen Maselle na maofisa wengine wa wizara, yalijikita zaidi katika sekta ya Nishati.

BREAKIING NEWSSSSS MAFISANGO WA SIMBA AFARIKI KWA AJALI YA GARI


KIUNGO wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Mutesa Mafisango wa Simba, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Tazara, Dar es Salaam.

Mafisango amefariki kwa ajali ya gari akiwa anarejea nyumbani kwake, kutoka disko na kwa sasa mwili wke upo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Meneja wa Simba SC, Nico Njohole amethibitisha kifo cha mchezaji huyo na amesema hilo ni pigo kubwa kwa klabu hiyo.

Mafisango aliyekuja nchini mwaka juzi na kujiunga na Azam kabla ya kuhamia Simba mwaka jana, alizaliwa Machi 7, mwaka 1987 Rwanda na kabla ya Tanzania alichezea APR ya Rwanda.

 Mechi ya mwisho Mafisango kuichezea SImba ilikuwsa dhidi ya Al Ahly Shandy Jumapili katika hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho, ambayo Simba ilitolewa kwa penalti 9-8, kufuatia sare ya jumla ya 3-3.

Hadi anafariki dunia, Mafisango alikuwa ni tegemeo na jana tu Makamu Mwenyekiti wa Simba, Geoffrey Nange Kaburu alisema kiungo huyo yupo kwenye mpango wa kocha wa kikosi cha msimu ujao.

TAMASHA LA TIGO LAPAGAWISHA WATU KARATU

Msanii  wa Muziki wa kizazi kipya,Hamis Baba maarufu kama H Baba akiwapagawisha mashabiki wake kwenye Kituo cha mabasi wilayani Karatu mkoa wa Arusha katika Bonanza lililoandaliwa na Tigo na kutoa zawadi kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria.Picha na mpigapicha wetu



 Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Hamis Baba maarufu kama H Baba(kulia) akiimba na kucheza na watoto waliojitokeza  kwenye Kituo cha mabasi wilayani Karatu mkoa wa Arusha katika Bonanza lililoandaliwa na Tigo na kutoa zawadi kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria.Picha na mpigapicha
 Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Hamis Baba maarufu kama H Baba(kulia) akiimba na kucheza na watoto waliojitokeza  kwenye Kituo cha mabasi wilayani Karatu mkoa wa Arusha katika Bonanza lililoandaliwa na Tigo na kutoa zawadi kwa wananchi mbalimbali waliohudhuria.Picha na mpigapicha

Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika lilivyorindima Uturuki

 Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (kushoto) akipokea tuzo maalumu kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Jamhuri ya Uturuki (Idara ya Habari na Maelezo), Murat Karakaya iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc aliyemwakilisha Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Recep Tayyip Erdogan, baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika. Picha zaidi Uk. 11. (PICHA NA MPIGA PICHA MAALUMU)
 Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
 Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc akifungua mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
 Mkurugenzi wa Raia Mwema aliyepata pia kuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo na Kampuni ya New Habari 2006, John Bwire (kushoto) na Kaimu Mhariri wa Makala wa Habari Leo, Selemani Nzaro wakifuatilia mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.
 Profesa, Dk. Mohamed Bakari, raia wa Kenya anayefundisha Chuo Kikuu cha Fatih nchini Uturuki, akipokea tuzo maalumu iliyotolewa kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu Uturuki, Bulent Arinc baada ya kuwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Afrika ya Leo: Sera za Siasa, Uchumi na Mambo ya Nje' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka nchi 54 za Afrika.

 Baadhi ya washiriki wakifuatilia wakati Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward (mbele kwenye video) akiwasilisha mada katika mkutano wa Jukwaa la Vyombo vya Habari Afrika na Uturuki kuhusu 'Vyombo vya Habari kama kichocheo cha ushindi wa vita dhidi ya migogoro na ugaidi' mjini Ankara, Uturuki wiki iliyopita. Mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya Waziri Mkuu Uturuki, ulishirikisha wawakilishi wa vyombo vya habari na wadau wengine kutoka

Wednesday, May 16, 2012

WAZIRI WA ZAMANI WA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII DKT. MPONDA AKABIDHI RASMI OFISI

 Waziri wa zamani wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hadji Mponda akimkabidhi kitabu cha sheria na mwongozo wa utendaji kazi wa wizara hiyo Waziri Mpya  Dkt. Hussein Mwinyi.Makabidhiano hayo yamefanyika leo kwenye ukumbi wa wizara hiyo
Mawaziri hao wakipeana mkono mara baada ya makabidhiano hayo Dkt. Mponda amemtaka waziri Dkt. Mwinyi kufuatilia na kusimamia vyema  utekelezaji wa  mikakati ya sekta ya afya ili kuweza kuimarisha huduma ya afya kwa wananchi
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Hussein Mwinyi aliyekaa katikati,Kulia ni waziri wa zamani Dkt. Hadji Mponda na Naibu Waziri Mpya Dkt. Seif Rashid aliyekaa kushoto, wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa wizara hiyo mara baada ya makabidhiano ya ofisi.(Picha na Catherine Sungura-Mohsw)

SUPER D BOXING COACH AKABIZIWA CHETI CHA KUTAMBUA UWEZO WAKE WA KUSAPOTI MASUMBI KUSONGA MBELE


Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' akipokea cheti kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime cha kutambua mchanmgo wake wakati wa Mpambano wa Francis Cheka na Mada Maugo SUPER D ambaye ni Kocha wa Masumbwi na Mtaalishaji wa DVD za masumbwi zinazofundisha sheria na mbinu za mchezo huo akichanganya na mabondia wa kimataifa

NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI KWA SHULE ZA MKOA WA MTWARA

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali (Mst) Joseph Simbakalia akisalimiana na Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo huku wakishuhudiwa na Meneja wa Mahusiano Bi. Shy-Rose Bhanji wakati wa kukabidhiwa msaada wa Madawati kwa Shule za Mkoa wa Mtwara.
(Picha zote na Beatha Hyera, Afisa Habari Mtwara)
 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Joseph Simbakalia (wa kulia) akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 15 kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Kusini Bw. Thomas Kilongo wakati wa kukabidhiwa msaada huo utakozinufaisha Shule za Msingi katika Wilaya za Masasi na Newala.
 Meneja wa Mahusiano Benki ya NMB Bi. Shy-Rose Bhanji akitoa maelezo kwa Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kuhusiana na msaada huo na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Benki ya NMB na wananchi kwa ujumla katika kuhakikisha maendeleo ya elimu katika nchi yetu

Rais Kikwete atembelea Ofisi za Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba jijini Dar es Salaam

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete jana alitembelea ofisi za Tume ya kukusanya na kuratibu maoni juu ya katiba zilizopo katika jengo jipya katika Wizara ya Mambo ndani jijini Dar es Salaam.Akizungumza na wajumbe wa Tume hiyo Rais Kikwete alirudia ahadi yake ya kuwapatia nyenzo za kazi ikiwemo usafiri ili kuiwezesha tume hiyo kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.Pichani Rais akizungumza na wajumbe wa tume hiyo katika ukumbi wa mikutano uliopo katika jengo la tume hiyo jana.
Mwenyekiti wa Tume ya Kuratibu maoni juu ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba(kulia) akizungumza na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati Rais alipomtembelea ofisi kwake jana.Wengine katika picha ni Makamu mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mkuu Mstaafu Mhe. Agostino Ramadhani(Watatu kushoto),Waziri wa Katiba na SheriaMhe. Mathias Chikawe(Wapili kushoto) na kushoto ni naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angela Kairuki.

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiteta jambo naProfesa Mwesiga Baregu ambaye ni mjumbe  wa Tume ya kuratibu maoni kuhusu katiba wakati Rais alipotembelea ofisi za tume hiyo jijini Dar es Salaam jana(picha na Freddy Maro).
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(Wanne kushoto Mstari wa mbele) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Tume ya kuratibu maoni  ya Katiba wakati alipotembelea ofisi za tume hiyo Jijini Dar Es Salaam jana.

Tuesday, May 15, 2012

MAMA SALMA AZINDUA 'OKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO'



Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya Mheshimiwa Dr. Hussein Mwinyi (kushoto),na Mkurugenzi wa Amref Dr. Festus Lakko (kulia) wakiangalia machapisho mbalimbali yanayohusiana na afya ya mama na mtoto kutoka shirika la Amref wakati wa uzinduzi rasmi wa 'Okoa maisha ya mama na mtoto. Changia mafunzo ya wakunga', au, stand up for African women. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja tarehe 15.5.2012.


Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia zawadi ya saa aliyopewa na uongozi wa Amref yenye ujumbe wa 'stand up for African women' mara baada ya kuzindua rasmi kampeni ya kuchangia mafunzo ya wakunga ili kuokoa maisha ya mama na mtoto barani Africa yaliyofanyika Mnazi mmoja jijini Dar tarehe 15.5.2012.

Mwenyekiti wa WAMA na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisaini katika kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya 'Stand up for African women' inayoratibiwa na Shirika la Amref. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam tarehe 15.5.2012. PICHA NA JOHN  LUKUWI